BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi wa kazi za sanaa Tanzania wiki hii lilitoa rai nzuri kwa wasanii wote na kazi zao.
Liliwakumbusha wasanii juu ya umuhimu wao kwa jamiii pana ya Watanzania kupitia kazi zao na hasa vita dhidi ya dawa za kulevya.
Basata liliwataka wasanii kuacha kutunga nyimbo zinazochochea matumizi ya dawa za kulevya na badala yake ziwe
na ujumbe unaopambana na dawa hizo.
Ni ujumbe mzuri kutoka chombo chenye dhamana ya kusimamia wasanii na maudhui ya kazi zao. Vijana ni kundi kubwa katika jamii linalofuatilia kazi mbalimbali za wasanii kupitia sanaa ya maigizo au nyimbo mbalimbali zinazotungwa.
Lakini pia, ni kundi kubwa kwenye jamii linaloendelea kuathirika na utumiaji wa dawa za kulevya na hivyo kulipotezea taifa nguvu kazi kubwa.
Kama kioo cha jamii wasanii wana dhamana kubwa ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kupitia kazi zao na
kwa kuwa wana ushawishi mkubwa, wanaweza kulisaidia taifa katika vita hii.
Wasanii wamebeba jukumu kubwa la kuirudisha jamii kwenye maadili yanayotakiwa na kupitia kazi zao wana nafasi
kubwa ya kupambana na aina yoyote ya mmomonyoko wa maadili, ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
Vita dhidi ya dawa za kulevya haiwezi kupiganwa na serikali pekee bali kila kundi lenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ya Watanzania, wakiwemo wasanii.
Jamii yenye maadili mema si rahisi kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya, hivyo ni sahihi ujumbe huu wa Basata kwa wasanii kwani ndio hasa unabeba utatuzi wa kiini cha tatizo kwa kunyoosha maadili kupitia kazi zao.
Kwa sababu suala la matumizi ya dawa za kulevya linahusisha tabia, ni suala la kimaadili zaidi hivyo sanaa ni njia
sahihi ya kuonya na kuelimisha jamii.
Kitendo cha Basata kuja na ujumbe huo kwa wasanii kinaashiria mambo mawili; mosi ni kwamba tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kwenye jamii ni kubwa na hivyo kunahitajika mchango wao kupambana nalo.
Lakini pili ni kwamba tungo au kazi zao nyingi pengine zimekuwa zikitoka nje ya mstari, kwamba badala ya kuwa
msaada kwenye kukabiliana na tatizo hilo, zimekuwa kichocheo kwa namna moja au nyingine kwenye matumizi ya dawa hizo za kulevya na hivyo kuwataka wabadilike.
Tunaamini ujumbe huu wa Basata utapokelewa vizuri na kuanza kushuhudiwa tungo au kazi zao nyingi zikipambana
na matumizi ya dawa za kulevya.
Undeniably believe that which you said. Your favorite justification appeared to be on the internet the easiest thing
to be aware of. I say to you, I definitely get irked while people consider worries that they just don’t know about.
You managed to hit the nail upon the top and also defined out the whole thing without having side effect , people
can take a signal. Will probably be back to get more.
Thanks