Bashe azindua kituo atamizi cha mkonge

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amezindua kituo atamizi cha mkonge ambacho kitakuwa ni eneo la ubunifu na uzalishaji wa bidhaa za mikono kwa kutumia singa za mkonge kwa lengo la kuleta matokeo ya haraka kwa wakulima na wafanyabiashara.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema lengo la serikali ni kuweka kituo katika Mkoa wa Tanga ambacho kitawekewa vifaa vidogodogo vya kuongeza thamani, mkonge na mazao mengine madogo madogo na kuweza kufikishwa na kuchakatwa bidhaa hicho.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha amesema kuwa kituo hicho kitakwenda kusaidia kukuza uchumi wa mkoa wa huo, hasa kwa kutumia kilimo cha mkonge na mazao yake.

SOMA: Bashe acharuka mabadiliko vyama vya ushirika

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mkonge na Masoko Bodi ya Mkonge Tanzania Olivo Mtung’e amesema kituo hicho kitakwenda kuwasaidia wakulima wa mkonge Tanga kupata sehemu ya kupeleka bidhaa yao,balada ya kutegemea kwenda nje ya nchi.

Habari Zifananazo

Back to top button