Bashungwa atoa maelekezo matengenezo barabara

MTWARA; Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ametoa siku nne kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) nchi nzima kufanya tathmini na ukaguzi wa madaraja, makalavati na barabara kuu zote, ambazo zimekuwa zikifanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na kuwasilisha taarifa hizo kwa wakuu wa mikoa, ili ziweze kuchukuliwa hatua ya haraka.

Agizo hilo amelitoa mkoani Lindi Machi 5, 2024 kutokana na taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa kuhusu matokeo ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali na kuathiri miundombinu ya barabara, madaraja na makalvati kwa baadhi ya maeneo.

“Nielekeze hadi kufika Machi 9 mwaka huu, kila Meneja wa Mkoa wa TANROADS na timu yake wakabidhi taarifa ya hali ya barabara na maeneo ya hatari yanayoweza kujitokeza katika madaraja na makalavati, ili serikali iweze kuchukua hatua za haraka,” amesema Bashungwa.

Habari Zifananazo

Back to top button