Bayern yataka kumng’ang’ania Jamal Musiala
TETESI za usajili zinasema Bayern Munich inahangaika kukubaliana vipengele vya mkataba mpya na Jamal Musiala, hali ambayo imetoa ahadhari kwa Manchester United kuhusu uwezekano wa kupatikana wake muda mfupi ujao.
Pia Manchester City na Real Madrid zina nia kumsajili nyota huyo wa kimataifa Ujerumani (Daily Mirror)
SOMA: Haaland aongoza kwa thamani, Saka, Vini Jr wafuata
Chelsea inaweza kufanya majaribio mapya kumsajili Victor Osimhen duriwakati wa dirisha la uhamishoi Januari 2025, licha ya uhamisho wake wenda Galatasaray kwa mkopo. (Football Insider)
Liverpool ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu England vinavyoaaminika kumfuatilia kiungo wa Lille, Angel Gomes.