Beatrice Alex ang’ara Miss Grand International

MWAKILISHI  wa Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International yanayoendelea kufanyika nchini Thailand, Miss Beatrice Alex, ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kushika nafasi ya 3 katika kipengele cha Grand Talk na nafasi ya 15 katika kipengele cha Talent, ambapo alitumbuiza kwa kucheza wimbo maarufu wa “Chambua kama Karanga” wa msanii Saida Karoli.

Mashindano hayo makubwa ya urembo yanatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 18, 2025 (Jumamosi), ambapo Beatrice ana nafasi kubwa ya kuingia Top 5 au hata kutwaa taji la Miss Grand International 2025.

Akizungumza na HabariLEO kwa njia ya simu kutoka Thailand, Beatrice amewaomba Watanzania kuendelea kumpa sapoti kwa kumpigia kura kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, ikiwemo Instagram, ili kuisaidia Tanzania kushinda taji hilo.

“Nashukuru Mungu kwa hatua hii niliyoifikia. Ni fursa ya pekee kwa Tanzania kuonekana kimataifa. Naomba Watanzania waungane nami kwa kunipigia kura kwa wingi, ili taji la Miss Grand 2025 lirejee nyumbani,” amesema Beatrice. SOMA: Miss Universe Tanzania 2025 wanogesha mambo

Beatrice alitawazwa kuwa Miss Grand Tanzania 2025 katika hafla ya kuvutia iliyofanyika usiku wa kuamkia Agosti 17, 2025, katika ukumbi wa Superdome uliopo Masaki, jijini Dar es Salaam. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25, ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo aliuwakilisha Mkoa wa Dar es Salaam katika shindano lililohusisha warembo 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Mbali na urembo, Beatrice anatambulika kwa kipaji chake cha kuchora, kupiga picha na kusafiri, pamoja na jitihada zake za kijamii katika kuhamasisha elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu, hasa wale wanaotoka katika familia zenye mazingira magumu.

Ameeleza dhamira yake ya kuona kila mtoto anapata fursa sawa ya elimu katika mazingira yanayozingatia mahitaji maalum, akisisitiza kuwa mafanikio yake katika jukwaa la kimataifa yatatumika kuinua sauti ya watoto wenye changamoto hizo. Kwa hatua hii, Beatrice Alex ameipa Tanzania nafasi adhimu ya kutambulika kimataifa, akibeba matumaini ya mamilioni ya Watanzania wanaomuombea ushindi katika fainali za Miss Grand International 2025.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button