Begashe afariki dunia

MANYARA: KOCHA wa Kimataifa wa  zamani wa mchezo wa Rihadha,  Jasson Begashe amefariki Dunia usiku wa kuamkia Januari 9, 2024 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Akizungumza na HabariLEO  Sixmund Begashe ambaye ni mtoto wa marehemu amesema baba yake atazikwa Ijumaa,Januari 12,2024  saa nane mchana, wilaya ya Babati Manyara nyumbani kwake.

Begashe mbali na kuwa kocha wa riadha, pia amewahi kuwa  Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania – TALGHU.

Akitoa historia ya marehemu, Sixmund  amesema Begashe  aliwezesha timu ya taifa ya mchezo huo kupata  heshima kubwa kupitia wanafunzi wake akiwemo mwanariadha wa Kimataifa Juma Ikangaa, John Bura na wengine wengi.

Alisema pamoja na mambo mengine Mzee Begashe mwaka 2010 akiwa Kaimu Katibu Mkuu wa TALGHU, atakumbukwa kwa ushirikiano wake mzuri na Serikali uliosababisha ongezeko kubwa kwa mishahara ya watumishi nchini.

Alisema katika uhifadhi wa maliasili na kukuza utalii nchini, Mzee Begashe alikuwa mmoja wa waasisi wa marathon kongwe hapa nchini, “Babati Half Marathon”, mjini Babati iliyovutia wageni wengi kutoka nje ya nchi, na pia kuwa chachu ya marathon nyingi hivi sasa nchini.

Alisema Begashe atakumbukwa zaidi na wafanyakazi wa Babati Manyara kwa kuimarisha michezo, uwasisi wa uwanja wa sasa wa Mpira mjini Babati, na hata ushiriki wake kwenye mambo ya kijamii

Habari Zifananazo

Back to top button