Benki ya Stanbic yamkabidhi gari Mtanzania

BENKI ya Stanbic imemkabidhi gari Mtanzania Edwin Shayo aina ya Suzuki Fronx baada ya kushinda kampeni ya Tap Kibingwa.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika eneo la kazi la mshindi huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.
Kampeni hiyo ilianza Januari hadi Aprili 2025, ikiwa na dhamira ya kutumia miamala bila pesa taslimu na kuwazawadia wateja waliotumia kikamilifu kadi zao za Debit za Visa kwa malipo ya kila siku.
Stanbic iliimarisha kichocheo cha ujumuishaji wa kifedha, uvumbuzi wa malipo, na suluhisho za kibenki zinazozingatia wateja.
Akizungumza wakati wa utaoji zawadi hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya , Shangwe Kisanji alisema Tap Kibingwa ni moja ya harakati zao za kuwasaidia watanzania kupata urahisi ba usalamaxwa malipo kidigitali.
“Leo tunasherehekea sio tu ushindi wa Edwin lakini maelfu ya wateja waliochagua kutumia huduma ya kidijitali mara kwa mara na bila kusita,” alisema Kisanji.
Aidha, Kisanji alisema kuwa kampeni hiyo inawiana kwa karibu na agizo la Benki Kuu la Tanzania la kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha za kidijitali na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu, hasa wakati taifa linavyozidi kushika kasi kuelekea uchumi shirikishi na unaoendeshwa na teknolojia.
“Kampeni hii inaunga mkono moja kwa moja malengo ya sekta ya fedha ya Tanzania. Stanbic, tunajivunia kuongoza mabadiliko haya. Tunaamini kufanya zaidi ya benki katika kuleta athari chanya,” Alisema
Katika muda wote wa kampeni, Stanbic ilitoa droo tatu za kila mwezi, kila moja ikiwazawadia wateja watano Sh 500,000. Kwa jumla, wateja 15 walipata Sh milioni 7.5 kama zawadi ya fedha taslimu.
Kwa kujibu wa benki hiyo matarajio yaliongezeka, huku zaidi ya asilimia 80 ya wateja wakishiriki na ongezeko la asilimia 20 la matumizi ya Visa Debit Card kwa wateja wa Stanbic.
Kivutio kikuu cha kampeni hiyo kilikuwa ni makabidhiano ya Suzuki Fronx ya mwaka 2024 yenye matumizi ya umbali usiozidi maili sifuri.
Edwin Shayo, aliyeweza kujishindia gari hiyo katika droo kuu kupitia matumizi yake ya mara kwa mara ya kadi ya thamani ya juu alisema gari hilo limekuwa baraka katika maisha yake.
“Zaidi ya kila kitu kwa sasa naona umuhimu wa kutokuwa na pesa taslimu. Ni matumizi ya Visa ambayo ni ya haraka, salama, na rahisi zaidi,” alisema.
Tap Kibingwa pia ni sehemu ya dhamira pana ya Stanbic inapoadhimisha miaka 30 ya kutoa huduma nchini Tanzania. Kwa ujumbe elekezi “Tanzania ni nyumbani kwetu, na tunachochea ukuaji wake,” Benki ya Stanbic inaendelea kuwekeza katika huduma zinazoinua uzoefu wa wateja, kuleta ufikiaji, na kusaidia mabadiliko ya kiuchumi.



