Benki yazindua akaunti maalum kuwainua wanawake wajasiriamali

KATIKA jitihada za kumkomboa mwanamke kiuchumi, Benki za Akiba (ACB) imezindua akaunti maalum kwa ajili ya wanawake wajasiriamali.

Akizungumza katika uzinduzi wa akaunti hiyo iliyopewa jina la ‘Waridi Akaunti’, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Dora Saria amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwawezesha wanawake wajasiriamali kutimiza ndoto zao kupitia benki hiyo.

Wafanyakazi wanawake wa ACB wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Huduma mpya ya AKAUNTI YA WARIDI ya wafanyazi wanawake wa Akiba Commercial Bank Plc katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Siku ya Wanawake Duniani katika ofisi za makao makuu jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umembatana na maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika hafla ndogo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo yaliyopo jijini Dar es salaam.

ACB imechukua uamuzi huo wa kuanzisha akaunti hiyo maalum huku Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ikisema kuwa wanawake wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto lukuki katika sekta ya kifedha kwani kwa sasa ni asilimia 7.8  ndio pekee wana uwezo wa kupata mikopo kutoka benki ikilinganishwa na asilimia 22 ya wanaume.

Changamoto nyingine ni masoko, kupata taarifa na ushiriki wao katika uchumi rasmi.

Habari Zifananazo

Back to top button