Biashara asubuhi jioni mahesabu

LEO ndio leo , usiku wa deni haukawiii , timu za Ligi Kuu Bara zitavuna zilichokipanda tangu kuanza kwa msimu mwa mwaka 2022/2023 ambapo pazia la ligi hiyo pendwa Afrika Mashariki na kati linafungwa rasmi.

Michezo yote ya mwisho itapigwa leo tena kwa wakati mmoja ambapo Bodi ya Ligi imesisitiza timu yoyote itakayobainika kuhusika kwenye kupanga matokeo  hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Wakati michezo hiyo ya mwisho ukisubiriwa kwa hamu Mabingwa wa ligi hiyo Yanga watakabidhiwa ubingwa wao huko jijini Mbeya, lakini pia mfungaji bora wa ligi hiyo atafahamika ambapo vita ni ya nyota wawili Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 na Saido Ntibanzonkiza wa Simba mwenye mabao 15.

Advertisement

Pastashika nguo kuchanika ipo huku timu tano bado hazina uhakika wa kuwepo kwenye ligi kuu msimu ujao , kuna chujio litapita  kwa timu zitakazomaliza kwenye nafasi ya 13 na 14.

Kati ya KMC au Mbeya City ni lazima mmoja wao acheze hatua ya mtoano kutokana na timu hizo kukutana wenyewe kwa wenyewe kwenye mchezo wa mwisho wa ligi kuu utakakaopigwa jijini Mbeya , mpaka sasa KMC wapo nafasi ya 14 wakiwa na alama 29 huku Mbeya City wakiwa nafasi ya 13 na alama 31.

Timu ya Mtibwa Sugar Coastal Union,Dodoma Jiji nazo hazina uhakika wakuwepo msimu ujao

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *