WASHINGTON DC: RAIS wa Marekani, Joe Biden (81) ametangaza kuondoka kwenye kinyang’anyiro cha urais na kusitisha kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, alisema jana kuwa atabaki katika nafasi yake kama rais hadi muhula wake utakapokamilika Januari mwakani na atalihutubia taifa wiki hii.
“Imekuwa heshima kubwa maishani mwangu kuhudumu kama rais wenu. Na ingawa imekuwa nia yangu kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa. Nitaendelea kutekeleza majukumu yangu kama rais kwa muda uliosalia wa muhula wangu,” Biden aliandika.
Amechukua uamuzi baada ya wanachama wenzake wa Democratic kupoteza imani na uwezo wake wa kumshinda Donald Trump kutokana na mdahalo kati yake na rais huyo wa zamani, ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya Republican.
Uamuzi huu wa Biden unatajwa kumfungulia njia Makamu wa Rais Kamala Harris kugombea urais akiwa mwanamke wa kwanza mweusi kufanya hivyo katika historia ya Marekani.
SOMA: Biden kugombea tena urais Marekani
I