MAREKANI : WAZIRIMKUU wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Marekani, Joe Biden, wamezungumzia jitihada zilizofanyika za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka katika vita vya Israel na Hamas.
Mazungumzo haya yanakuja ikiwa zimebaki siku chache kabla ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuingia madarakani wiki ijayo. SOMA: Biden: Marekani inasimama na Israel
Wapatanishi kutoka Marekani, Qatar, na Misri wamekuwa wakifanya mazungumzo juu ya kusitisha mapigano tangu mwaka jana, lakini bila mafanikio.
Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Israel, Mossad, David Barnea, pamoja na Mshauri Mkuu wa Rais Biden kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati, Brett McGurk, wako mjini Doha, Qatar kwa mazungumzo.
Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema anatumai makubaliano hayo yatapatikana kabla ya kukabidhi ofisi kwa utawala mpya chini ya Trump.