Bigman FC waitangazia maumivu Simba

DAR ES SALAAM; TIMU ya Bigman FC imetamba kuwa itadhihirisha ukubwa wake kesho watakapocheza na Simba mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB hatua ya 16 bora.
Ofisa Habari wa Bigman FC, Idrissa Sechambo amesema leo kuwa vijana wake wamejipanga tayari kwa mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam.
“Ili uthibitishe ukubwa ni lazima umshinde anayeaminiwa ni mkubwa, Bigman FC tunakwenda kuthibitisha ukubwa wetu mbele ya Simba SC,” ametamba.



