Bil 300/- zatumika pembejeo za korosho

SERIKALI imesema katika kipindi cha miaka mitatu imetumia zaidi ya Sh bilioni 300 kusaidia pembejeo za korosho nchini.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa wadau wa korosho mwaka 2024, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema jambo la msingi katika hilo ni kuanza kuwandaa wakulima na njia pakee ya kuondoa matatizo ni kutengeneza mfumo wao wa kusaijli wakulima uwe wa uhakika.

SOMA: Rais Samia aipaisha korosho Afrika

‘’Vyama vya ushirika vishiriki, serikali ya wilaya ishiriki, wakurugenizi kwani sosi yetu ni mazao, sasa ili kujihakikishia ni kuwajua wakulima wenu na ili uwajuwe wakulima na kupata takwimu sahihi ni lazima muusimamie mfumo wa usajili wa wakulima’’

Ameongeza kuwa: ‘’Kabla sijaanza kuhangaika na mageti ningeanza kuhangaika kumjua mzalishaji wa korosho, ufuta na mbaazi kwenye halmashauri yangu ni nani ana shamba kubwa, kiasi gani mwaka jana alizalisha.”

Aidha amewataka maofisa kilimo nchini kwenda kusimamia mfumo huo wa kusajili wakulima kwani utaisaidia serikali kuu kuonodokana na upotevu wa pembejeo ambapo katika msimu wa kilimo uliyopita mwaka 2023/2024 uzalishaji wa korosho nchini ulikuwa ni zaidi ya tani 300,000.

SOMA: Mbegu mpya 16 korosho, karanga zagunduliwa

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wote wa mikoa inayolima korosho, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amempongeza waziri huyo wa kilimo kwa usimamizi wake mzuri kwenye sekta hiyo kwani wameweza kujionea mabadiliko makubwa katika mazao mbalimbali ikiwemo zao hilo la korosho, ufuta na mbaazi hasa usimamizi nzuri wa masoko.

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Selemani Sankwa ameipongeza serikali kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania hususani wakulima wa zao hilo.

Akitoa salamu kwa niaba ya wadau wa korosho nchini, mwenyekiti wa mkutano mkuu wa wadau wa korosho nchini, Yusufu Nannila ameipongeza serikali kwa jitihada zake kubwa inayofanya kwenye tasnia hiyo hasa ile hali ya kukitoa kilimo hicho kutoka kwenye kilimo cha kujikimu hapo awali na kuwa kilimo cha biashara kwa sasa.

Habari Zifananazo

Back to top button