Bil 4.4/- kuweka historia huduma za maji Kibondo

SHILINGI Bilioni 4.4 zilizotolewa na serikali kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kibondo (KIWASA) zimeandika historia kwa wakazi wa mji huo ambao walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Meneja wa KIWASA, Mhandisi Aidan Ngatomela amesema hayo akitoa taarifa kwa mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Abdulkadri Mushi aliyeongoza kamati ya siasa ya CCM mkoa Kigoma kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kibondo.

Ngatomela amesema kuanzia mwaka 2020 KIWASA ilianza kupokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo upatikanaji wa maji ukiwa asilimia 46 lakini sasa umeongezeka na kufikia asilimia 75.

Amesema kazi kubwa iliyofanyika ni uboreshaji wa vyanzo vya maji, ujenzi wa chujio la kusafishia maji, utandazaji wa miundo mbinu ya maji kwenda kwa wananchi na kwa sasa mamlaka inamalizia ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 1.5.

Ngatamela amesema hatua hiyo itaondoa changamoto za upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Kibondo na huduma itafikia asilimia 85.

Akihitimisha ziara ya kutembelea mradi huo Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Abdulkadri Mushi amesema chama hakitaki taarifa na hotuba nzuri za wataalam na viongozi bali taarifa hizo ziishi katika maisha halisi ya mtanzania kuhakikisha huduma inayotolewa taarifa inanufaisha wananchi na utekelezaji wa mradi husika huku akipongeza utekezaji wa mradi huo wa Kibondo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button