Bilionea Mustafa Sabodo afariki Dunia

Kuzikwa leo saa 4:30 usiku - Dar es Salaam

DAR ES SALAAM: Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam, mtoto wa marehemu, Danstan ameiambia Daily News Digital.

“Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE,” amesema Danstan.

Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.

Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.

Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button