Bint wa Sierra Leone aokolewa baada ya siku tatu baharini

ITALIA : BINTI mmoja mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni  raia wa Sierra leone ameokolewa katika ajali ya boti baada ya kukaa kwa siku tatu baharini katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

Shirika la uokoaji nchini Ujerumani limesema wafanyakazi wake wa meli waliokuwa njiani kuelekea kwenye tukio jingine la dharura, walisikia sauti baharini ya mtoto huyo majira ya saa tisa alfariji.

Aliokolewa akiwa amevalia jaketi maalum la kumsadia kutozama huku akiwa anaelea baharini akiwa juu ya boya la kuogelea. SOMA: Wahamiaji haramu 25 wapoteza maisha Comoro

Binti huyo amedai kuwa  alisafiri na watu wengine kutoka  mji wa Sfax Tunisia kwa boti ya kuundaunda akiwa na watu wengine 45 ambayo ilizama kutokana na dhoruba kali baharini.

Habari Zifananazo

Back to top button