Biteko aagiza Meneja Tanesco asimamishwe kazi

MTWARA; NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (tanesco), kumsimamisha kazi Meneja wa Huduma kwa wateja kwenye shirika hilo na kuweka mtu mwingine kufanya hiyo kazi.

Pia amemuahiza Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kumuondoa mara moja kazini Ofisa Uhusiano na kuweka mtu mwingine kwa kushindwa kufanya kazi yake.

Biteko ametoa maagizo hay oleo Novemba 14, 2023, wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Msimbati, Halmashauri ya Mtwara, mkoani Mtwara.

Amesema Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanesco, amekuwa akitoa majibu yasiyoridhisha kwa wateja pindi wanapopiga simu kwenye shirika kupata majibu kutokana na tatizo la umeme.

“Tanesco tuna kitengo cha huduma kwa mteja , ni kweli tuna changamto ya umeme, lakini watu wakipiga simu majibu wanayojibiwa wananiandikia meseji, wanalalamika wakisema majibu tunayopewa waziri sio yenyewe,” amesema.

Biteko ambaye alioneshwa kukerwa na mwenendo wa meneja huyo wa huduma kwa wateja amesema ni lazima watendaji serikalini wawajibike ipasavyo.

“Nimemuelekeza Mkurugenzi wa Tanescoi yule Menejea wa huduma kwa wateja pale Tanesco ondoa mara moja, weka mtu mwingine,” amesema na kuongeza:

“Lazima tuheshimiane kazi ifanyaike, wananchi wanataka umeme, watu wanataka gesi, watu wanataka gesi ibadilishe maisha yao, hatuwezi kuja hapa tumevaa tumependeza watu wanalia shida ndogo ndogo,” amesema.

Kwa upande wa Ofisa Uhusiano TPDC, Biteko amesema ameshindwa kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa , kusikiliza kero kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya miradi ya gesi nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
17 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Scholarship ya Mwanadamu mwenye
Scholarship ya Mwanadamu mwenye
16 days ago

Scholarship ya Mwanadamu mwenye akili ya ‘Kinyonga mdogo zaidi duniani’ aliyegundulika Tanzania

Kinyonga kwa jina Brookesia urefu wake ni milimita 13.5

Wanasayansi wanaamini kuwa wamebaini kinyonga mdogo zaidi duniani ambaye ukubwa wake ni sawa na mbegu.

Vinyonga hao wawili ilibainika nchini Madagasca na timu ya sayanasi ya Ujerumani na Madagasca.

Kinyonga wa kiume aliyepewa jina la Brookesia urefu wake ni milimita 13.5.
Na kinyonga huyo anakuwa mdogo zaidi kati ya spishi karibu 11,500 za vinyonga, kulingana na rekodi ya hifadhi ya wanyama ya taifa ya Bavaria katika mjini mkuu wa Munich.

Urefu wake kutoka juu hadi chini ni milimita 22.
Kinyonga wa kike ni mkubwa kidogo takribani milimita 29, taasisi hiyo imesema, ikiongeza kwamba aina nyingine bado hazijapatikana, licha ya kwamba “juhudi zimekuwa zikiendelea”.

“Kinyonga huyo mpya aliyepatikana kaskazini mwa Madagascar eneo la msitu linalopokea mvua kubwa, huenda yuko katika hatari ya kutoweka,” kulingana na jarida la wanasayansi.

Oliver Hawlitschek, mwanasayansi wa kituo historia huko Hamburg, alisema: “Kwa bahati mbaya eneo alilokuwa akiishi mjusi huyo lilianza kuingiliwa na binadamu lakini likaanza kulindwa hivi karibuni, kwahiyo anawezaa kunusurika.”

Watafiti walibaini kwamba kinyonga huyo alikuwa anatafuta mchwa katika msitu wenye mvua kubwa na kujificha dhidi ya wanyama wala nyama usiku kwenye nyasi.
Katika msitu ambao mjusi Brookesia alipatikana umepakana na misitu mingine kaskazini mwa kisiwa, walisema.

Katika ripoti yao, wanasayansi wamependekeza kuwa kinyonga huyo aorodheshwe kama mnyama aliye hatarini katika orodha ya Shirika la IUCN, linalochunguza hali ya maelfu ya jamii za wanyama kumsaidia kumlinda na makazi yake.

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x