Biteko ataka watumishi ubalozini wachape kazi

KAMPALA, Uganda: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona Tanzania ikipiga  hatua kiuchumi na kuwataka wafanyakazi kumsaidia kutimiza azma hiyo.

Dk Biteko amesema hayo, Oktoba 10, 2023 alipozungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda ili kupeana taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii yanayoendelea nchini.

“Fanyeni kazi kwa uadilifu na Mheshimiwa Rais anathamini Sana mchango mnaoutoa kama ubalozi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza uchumi” Amesema Dk Biteko.

Akitoa tathmini juu ya masuala ya Nishati hususani Kuhusu masuala ya umeme, Dk Biteko amesema miradi yote ya kimkakati iko kwenye hatua nzuri na kutolea mfano wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kuwa litaondoa  changamoto ya upungufu wa umeme na kuwezesha vituo vya kuzalisha umeme wa maji kufanya matengenezo na kuongeza pia kiwango cha gesi ili kufidia mapungufu yaliyopo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi amewataka wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini  Uganda kuhakikisha wanatumia vema  fursa za kibiashara zilizopo nchini Uganda kwa manufaa ya nchi yetu na kuongeza ushirikiano wa kibiashara na wadau wote.

Amesema, takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka 2022 uwekezaji kwenye masuala ya biashara ulikuwa karibu shilingi bilioni 138  kutoka Tanzania pekee na kuwa nchi ya tatu kwa uwekezaji nchini Uganda.

Kikao hicho kimedhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Uganda.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Royal
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by. follow instructions on this website…….. http://Www.SmartCash1.com

money
money
1 month ago

Utaongea mwenyewe kuwa KAFA LAKINI ALIJENGA GOROFA MTAA WA SABA HISTORIA YAKE TAYARI IMEANDIKWA 2023..
file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg
MAANA YAKE KUFA KWA NGOMA AU MUUWAJI ANA MAANA/NGUVU/MAONO KULIKO RAIS

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x