Bodaboda wapongezwa ushiriki afya bonanzi 2025

MANYARA: Shirika la RAFIKI Wildlife Foundation lenye makao yake Wilaya ya Babati mkoani Manyara limesema afya bora huanza kwa kufanya mazoezi ya viungo yanayosaidia kujenga urafiki, undugu na kuondoa tofauti za kimitazamo.
Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI Wildlife Foundation,Clement Matwiga amesema hayo katika tamasha la Boda Boda Afya Bonanza 2025 lililofanyika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara mwishoni mwa wiki.
Amesitiza kuwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa la kuwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
”Tamasha hili limelenga utoaji wa elimu ya afya, uhamasishaji wa vijana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,utii wa sheria na usalama barabarani na kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa washindi wa mashindano wa maafisa usafirishaji,”mesema Matwiga.