Bugando yazindua kliniki ya madakatri bingwa

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando imezindua kliniki mpya ya madaktari bingwa na bingwa bobezi ‘Bugando Specialized Polyclinic’ kwa lengo la kuongeza na kuimarisha huduma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando, Fabian Massaga ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo iliyopo kata ya Isamilo mkoani Mwanza iliofanyika leo Machi 4, 2023.

‘’Bodi ya uendeshaji iliuagiza uongozi wa hospitali yetu kuanza kutafuta eneo ambalo lingefaa kwajili ya kufungua kliniki ya madaktari bingwa na bingwa bobezi ndani ya jiji la Mwanza’’ amesema Dk Massaga.

Amesema Oktoba 2021 walifanikiwa  kukodi jengo na kuanza ukarabati kwajili ya kliniki ya madaktari bingwa. Amesema  wazo lingine la kuanzisha kliniki hiyo ya kisasa  ni kutokana na ongezeko la idadi kubwa la watumishi takribani 1700.

Amesema kwa sasa hospitali yao inapokea wagonjwa 810 kwa siku na kwa mwezi inapokea wagonjwa 24400 kwa mwezi . Amesema kwa sasa kengo lao ni kupokea wagonjwa 30000 kwa mwezi. Ameeleza ukarabati, ununuzi wa mashine za kisasa,dawa, vifaa tiba na uwekezaji mzima uliofanyika ni umegharimu Sh bilioni 2.

Kliniki hiyo ina vyumba 17 vya kuhudumia wagonjwa wa binafsi,chumba kimoja cha kuhudumia wagonjwa wa VIP na chumba kimoja cha kufanyia matibabu mbalimbali na  chumba cha watalamu wa mifumo ya kielektroniki. Ina maabara ya kisasa, famasi yenye dawa zote muhimu zinazohitajika, vipimo vya radiololjia pamoja na moyo.

Amesema katika kliniki hiyo huduma zote zinatolewa kwa mfumo wa kielektroniki. Amesema kliniki hiyo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa.

Habari Zifananazo

Back to top button