Bukombe: Shughuli za uchimbaji zarejea Msasa

GEITA: SERIKALI imeruhusu shughuli za uchimbaji kuendelea katika mgodi wa Msasa wilayani Bukombe baada ya kubaini idadi kubwa ya wachimbaji wadogo hawana mgogoro na mmiliki wa leseni.

Azimio hilo linakuja siku chache baada ya kuripotiwa mgogoro uliotokana na utaratibu wa mgawo wa asilimia 50 kwa 50 kati ya mmiliki wa leseni na wachimbaji wadogo mgodini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesoma maazimio hayo ikiwa ni siku mbili baada ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita na wachimbaji wadogo wa mgodi.

Amesema kamati imeamuru shughuli za uchimbaji ziendelee chini ya sheria na taratibu za madini pamoja na makubaliano ya kimkataba kati ya wachimbaji na mmiliki wa leseni.

Amesema uamuzi huo unalenga kulinda maslahi ya watanzania wengi kwani kati ya maduara 1,344 mgodini hapo ni maduara 324 pekee sawa na asilimia 25 yapo ndani ya uzio wa mmiliki wa leseni.

Amesema pia tathimini imebaini kuwa wamiliki wa maduara 273 yaliyopo ndani ya uzio, sawa na asilimia 84 tayari walishakubali kusaini mkataba wa mgawo wa asilimia 50 kwa mmiliki wa leseni.

Ameeleza, ni wamiliki wa maduara 51 pekee yaliyopo ndani ya uzio sawa na asilimia 16 ya maduara 324 ndio wamebainika kuwa na mgogoro na hawajasaini mkataba wa mgawo wa asilimia 50.

Amesema kwa mantiki hiyo jumla ya wamiliki wa maduara 1,293 ikiwemo 1,020 walio nje ya uzio na wale 273 wa ndani ya uzio na walishasaini mkataba hawana mgogoro na mmiliki wa leseni.

Amesema kupitia tathimini hiyo utaratibu wa mgawo wa asilimia 50 kwa 50 utaendelea kama kawaida lakini mmiliki wa leseni atatakiwa kuchangia gharama za uzalishaji kwa kila duara.

Shigela amesema azimio lingine ni kuwa kamati imeagiza maduara yote ya wachimbaji yaliyo kwenye hifadhi ya barabara mgodini hapo yaendelee kufungwa kulinda usalama wa barabarani.

Amesema hatua hiyo inadhamiria kusimamia sheria ya ulinzi wa maeneo ya hifadhi ya barabara inayoagiza shughuli za uzalishaji zifanyike umbali wa mita 30 kutoka eneo la arabara.

“Wale ambao wapo nje ya hifadhi ya Barabara, tunatoa maelekezo kwa mmiliki wa leseni na ofisa madini mkazi, wasimamie chini ya Tanroads kuweka mipaka”, amesema Shigella.

Aidha Shigela amesema halmashauri imeagizwa kushughulikia changamoto za tozo za wafanyabiashara huku akifungua milango kwa watu ambao hawajarizishwa na uamuzi huo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button