KENYA : BUNGE la Kenya limekubali kujadili hoja inayohusu kumuondoa madarakani Makamu wa Rais Rigathi Gachagua kwa madai ya kukiuka katiba ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Spika wa Bunge Kenya amesema kwa maelezo yaliyowasilishwa Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amekuwa na mivutano na Rais William Ruto katika utekelezaji wa majukumu yake.
Zaidi ya thuluthi moja ya wabunge wamesaini hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge Mwengi Mutuse anayeegemea kambi ya muungano wa Rais Ruto.
Muungano huo unamtuhumu Gachagua kuwa anawanyima watu fursa za kupata uteuzi wa nafasi za umma na rasilimali.
SOMA: Mbivu mbichi kujulikana leo Kenya
Mpasuko kati ya Ruto na Gachagua umekuwa ukionekana waziwazi katika siku za hivi karibuni nchini Kenya, huku makamu huyo wa rais akisema ametengwa katika shughuli za kiserikali.