Bunge latoa maazimio 13 tija ya masharika

BUNGE limetoa maazimio 13 likiwemo la kuitaka serikali iweke utaratibu wa kutoa vibali kwa taasisi zinazojiendesha kibiashara ziajiri zenyewe ili zimudu soko la ushindani wa kibiashara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Silaa alisema hayo bungeni Dodoma wakati wa kuwasilisha maazimio hayo.

Alisema hatua hiyo itaindoa changamoto ya kupata vibali vya kuajiri hasa kwa mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara yanayokabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi katika kujiendesha kwake kutokana na kutegemea mchakato wa ajira unaoendeshwa na Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma.

Advertisement

Pia Bunge limeazimia serikali ikamilishe uteuzi wa wajumbe wa bodi 12 kwenye wizara 9 ambazo Rais ameshateua wenyeviti ndani ya miezi 3 na Serikali ikamilishe uteuzi wa wajumbe wa bodi 23 kwenye wizara 12 ambazo hazina bodi ndani ya miezi 6.

Alisema pia serikali ihakikishe inatimiza utaratibu wa kuanza maandalizi ya uteuzi wa bodi miezi tisa kabla bodi haijamaliza muda wake.

Kuhusu mikopo chechefu, Bunge limeazimia kwamba serikali ifanye tathmini ya madeni hayo na kuhakikisha wanaondoa kwenye vitabu vya benki hizo, bila kuathiri ulipaji wa mikopo inayolipika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *