Buriani Mwalimu Jenista Mhagama

WILAYANI Peramiho mkoani Ruvuma ndipo safari ya Jenista Joackim Mhagama ilipoanzia, tarehe 23 Juni 1967 alipozaliwa. Kisha safari yake ikahamia kwenye darasa la udongo la shule ya msingi hadi kuwa mwalimu, mwanasiasa, na hatimaye mmoja wa viongozi wanawake wenye ushawishi mkubwa katika Serikali ya Tanzania.

Jenista alianza elimu ya msingi mwaka 1976 katika Shule ya Msingi Mfaranyaki, kisha kuendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Wasichana Peramiho. Baadaye alijiunga na Chuo cha Mafunzo ya Ualimu Korogwe, ambako alisoma kidato cha tano na sita sambamba na mafunzo ya ualimu, na kuhitimu mwaka 1989.

Kutokana na kiu ya maarifa, aliongeza elimu kupitia stashahada na vyeti mbalimbali vya uongozi, usimamizi na ujasiriamali ndani na nje ya nchi. Mafunzo hayo yalimwezesha kujitengenezea nafasi katika uongozi, kipindi ambacho wanawake wachache walikuwa wakipata nafasi hizo. SOMA: Jenista ashitukia mfumo Tehama hospitali ya rufaa

Miaka sita ya kufundisha katika shule za sekondari ilimjengea nidhamu, uwezo wa mawasiliano na moyo wa kujitolea kwa jamii. Haikupita muda mrefu uwezo wake ukaonekana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alichojiunga nacho mwaka 1987 kama kada mchanga. Kuanzia nafasi ya katibu wa tawi, mjumbe wa baraza la wilaya, hadi uongozi wa UWT ngazi ya kata, Jenista alipanda ngazi hatua kwa hatua hadi kufikia majukwaa ya juu ya kisiasa.

Mwaka 2005 aliandika ukurasa mpya katika maisha yake baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, hatua iliyomvusha rasmi kwenye uongozi wa kitaifa. Katika Serikali ya Tanzania, Jenista amewahi kushika nafasi kadhaa muhimu, ikiwemo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu); Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, pamoja na Waziri wa Afya, nafasi aliyoihudumu hadi mwaka huu kabla ya uchaguzi wa 2025.

Uteuzi wake katika sekta ya afya uliambatana na jukumu kubwa la kufanya mageuzi, hususan katika maboresho ya mifumo ya afya, usimamizi wa taarifa na upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi.
Umahiri wake ulimfikisha pia kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Masuala ya Afya ya Ukanda wa Afrika Mashariki, jukumu linalomtambulisha kimataifa kama kiongozi mwenye mtazamo wa kikanda.

Nje ya majukumu ya serikali, Jenista ni mama wa watoto watatu. Ni mjane ambaye ameendelea kushinda changamoto za maisha kwa nguvu na hekima, akionesha mfano wa mwanamke shupavu anayesimama imara kati ya familia, kazi na taifa. Historia yake inaonesha misingi imara aliyojengewa na wazazi wake waliompa nidhamu, heshima na misimamo thabiti ambayo imekuwa dira katika maisha na utumishi wake.

Katika safari yake yote, Jenista Mhagama amejijengea taswira ya mwanamke aliyepanda ngazi hatua kwa hatua bila kuogopa changamoto. Ni taswira inayowapa mabinti wa Tanzania matumaini na mfano hai kwamba uongozi si zawadi ya kuzaliwa, bali ni matokeo ya bidii, msimamo na kujitolea kwa jamii. Leo hii Jenista Mhagama hatunaye tena, amefariki dunia akiwa anaumri wa miaka 58, miaka ambayo itaendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake mkubwa alioweza kuutoa kwa Taifa la Tanzania.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Job description
    JOB DETAILS:
    You would be responsible for:
    Scope of work:
    Broad objective:
    1. To conduct a qualitative study to identify the exposure, risk factors, and opportunities
    for improved responses for GBV affecting girls, adolescents, youth, and women with
    disabilities related to unpaid care activities carried out by caregivers and other social actors.
    2. Develop a policy brief with evidence informed recommendations and roadmap to
    strengthen the capacity of carers to address stigma and discrimination and prevent and respond
    to GBV and promote protection measures for women and girls who are survivors of GBV for
    adoption at national level.
    Specific objectives:
    Docusign Envelope ID: E588C253-1234-4D38-BBB7-AD82F21A7E39 Docusign Envelope ID: E62B7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button