Burkina Faso yaja Tanzania kujifunza Sekta ya Madini

TANZANIA imeendelea kuimarisha na kuthibitisha nafasi yake kama kitovu cha maarifa na uzoefu katika usimamizi na uendeshaji wa Sekta ya Madini barani Afrika, baada ya kupokea uumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta hiyo.
Ujumbe huo umepokelewa katika Ofisi za Wizara ya Madini Mtumba, Dodoma, ukiongozwa na Mshauri wa Masuala ya Uchumi, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Nishati, Madini na Machimbo (Ministry of Energy, Mines and Quarries) ya Burkina Faso, Halidou Ouedraogo.

Katika mazungumzo hayo, Wizara ya Madini, iliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchimbaji Mdogo, Eng. Moses Kongola akimwakilisha Kamishna wa Madini.
Akizungumza katika kikao hicho, Eng. Kongola alieleza kwa kina mageuzi yaliyofanywa na Serikali katika kuimarisha usimamizi, urasimishaji, na uendelezaji wa wachimbaji wadogo, usimamizi wa mazingira pamoja na kuboresha mazingira ya biashara katika Sekta ya Madini.

Alibainisha kuwa Tanzania imewekeza kimkakati katika kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuweka Sera madhubuti, Sheria na Kanuni rafiki kwa uwekezaji, pamoja na kuhamasisha uongezaji thamani wa madini ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo, Halidou Ouedraogo alisema Burkina Faso imevutiwa na hatua za Tanzania katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji, kuanzisha mifumo ya kusaidia wachimbaji wadogo kuingia katika uchimbaji rasmi, na kuunganisha Sekta ya Madini na maendeleo ya uchumi wa ndani.

Aliongeza kuwa ziara hiyo inalenga kujifunza kwa vitendo ili kuboresha Sera, mifumo ya usimamizi, na mikakati ya maendeleo ya Sekta ya Madini nchini Burkina Faso.
Aidha, ujumbe wa Burkina Faso utakaa nchini kwa muda wa siku sita, ambapo pamoja na vikao vya kitaalamu na Wizara ya Madini, utatembelea mikoa na maeneo mbalimbali ya shughuli za madini ikiwemo Tabora, Kahama (Buzwagi) na Geita Gold Mine.

Ziara hizo zinalenga kuwapa wajumbe fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu usimamizi wa shughuli za uchimbaji.




Kutana na Madini yaliyofichwa na Wachina Wakati wanajenga Reli ya TAZARA… Katika mto Njombe mkoa wa Njombe zamani ulikuwa IRINGA
https://youtube.com/shorts/E32eZcTDYTs?si=Y5wEiId0qFVHp4xN
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Kutana na Madini yaliyofichwa na Wachina Wakati wanajenga Reli ya TAZARA… Katika mto Njombe mkoa wa Njombe zamani ulikuwa IRINGA.
https://youtube.com/shorts/E32eZcTDYTs?si=Y5wEiId0qFVHp4xN
Start working at home with Google! It’s by-far the best job I’ve had. Last Wednesday I got a getting a check for $19400 this – 4 weeks past. I began this 8-months ago and immediately was bringing home at least $220 per hour. I work through this link, go to tech tab for work detail..
Open This Website——≻≻≻≻≻www.hot.cash54.com
I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
Start working at home with Google! It’s by-far the best job I’ve had. Last Wednesday I got a getting a check for $19400 this – 4 weeks past. I began this 8-months ago and immediately was bringing home at least $220 per hour. I work through this link, go to tech tab for work detail..
Open This Website——≻≻≻≻≻ww.hot.cash54.com
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. www.join.work27.com
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do…………………………………………………………………………………. www.join.work27.com