CAG abaini hasara mashirika 14

MASHIRIKA 14 ya umma ya kibiashara yamepata hasara katika uendeshaji. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonesha.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Charles Kichere amesema utafiti huo ni katika tathmini ya miaka miwili.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Sh bilioni 22.8 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 31.2. Kampuni ya Mkulazi ilipata hasara ya Sh bilioni 5.8 mwaka 2020/21 na mwaka uliofuata ilipata hasara ya Sh bilioni 14.3.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilipata hasara ya Sh bilioni 26.3 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 11.9.

Kwa mwaka 2020/21, Shirika la Ndege nchini (ATCL) ilipata hasara ya Sh bilioni 36.1 na mwaka 2021/22 Shirika lilipata hasara ya Sh bilioni 35.2.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button