CAG Kichere: Michezo tiba isiyo na gharama

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ametoa rai kwa watumishi wa umma wakiwemo wa Ofisi yake kushiri kwenye michezo kwani ni tiba isiyo na gharama.

Kichere ameyasema hayo wakati wa bonanza ambalo limefanyika sambamba na uchagiaji wa damu ikishirikisha pia watumishi wa taasisi zingine.

­

Advertisement

Taasisi zilizoshiriki mbali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mfuko wa Bima ya Afya ya Uchaguzi(NHIF), Wakala wa Barabara(Tanroads) Ofisi ya Rais Ikulu.

Alisema ili kuwa na afya njema ni vyema watumishi wakashiriki mazoezi na kusisitiza kuwa mazoezi ni tiba isiyo na gharama kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na pia kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia magonjwa hayo.

“Kazi zetu sisi Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali tunatumia muda mwingi kuandika taarifa hivyo tumekuwa tukiweka utaratibu wa kutoka nje kufanya mazoezi na ni utaratibu mzuri katika kulinda afya za watumishi.”

Kichere pia alisema wanatumia bonanza Hilo kujiandaa tayari na bonazan lingine litakalokutanisha na wabunge.

” Wabunge ni watu ambao tunafanya kazi nao kwa karibu, hivyo mwezi ujao tutakuwa na bonanza la kushirikiana na wabunge kwa hiyo hii ni sehemu ya mazoezi yetu.”

Kichere alisema katika bonanza Hilo pia watalitumia kuchagia damu benki ya Taifa ya damu Ili kusaidia kutoka maisha ya watu wanaohitaji damu.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya CAG, Novat Mfalamagoha kutokana na mtindo wa maisha ya mwanadamu mazoezi ni mabadala mzuri wa dawa za hospitali.

Pia alishauri wazazi kujenga tabia ya kuwashirikisha watoto kwenye mazoezi ambayo itawanyaka kujenga moyo wa kupenda mazoezi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *