CCM  Buguruni wamwangukia Rais Samia

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Buguruni wamemuangukia Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu na kumuomba kuitupia jicho Kata ya Buguruni kwa kuwaongezea fedha za miradi ya maendeleo
Ombi hilo limetolewa leo Januari 30, 2021 na Mwenyekiti wa  CCM kata ya Buguruni Mwishehe Rajabu mara baada ya  kukagua miradi inayotekelezwa na serikali katika Kata hiyo.
Mwishee ambae aliongozana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho Kata ya Buguruni pamoja na Viongozi wa CCM wa kata hiyo,  wametembelea miradi ya ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari, mradi wa ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua pamoja na mradi wa ufyatuaji wa matofali wa kikundi cha Wajane (MAHAME) ambao wamekopeshwa mkopo kutokana na fedha zinazotolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo kikundi hicho kilipewa asilimia nne ambayo ni shilingi milioni 200
Akizungumza Mwishehe anasema, Buguruni inapaswa kuangaliwa vizuri kwenye mgao wa fedha Kwa kuwa Kata hiyo inakusanya mapato mengi zaidi katika halmashauri ya Dar es salaam
“Kata yetu inakituo cha ukusanyaji wa mapato na wafanyabiashara walio wengi wa kata ya buguruni  ndio wanaokusanya hayo  mapato.
“Kwa mujibu wa taarifa yetu tumeonekana tumekusanya zaidi ya Shilingi milioni 200 kwa mwaka  lakini mgawanyo tunaopewa hauzidi asilimia 10, tunaiomba halmashauri ya jiji la Dar es salaam na serikali Kuu waturejeshee mgao wa  kutosha ili tuweze kutekeleza miradi mingi ya maendeleo”. Amesema
Amesema miradi waliotembelea yote kwa asilimia kubwa ipo kwenye hali nzuri ila bado mradi mmoja ambao wataendelea kuujadili na  kuweza kupata majibu ambao ni mradi wa TASAF ukiwa una sintofahamu hasa kutokana na fedha zilizotengwa hazilingani na maendeleo yaliyopo kwenye mradi huo.
Nae, Diwani Kata ya Buguruni Busoro Pazzi amesema katika kipindi kifupi, Kata ya Buguruni wamepatiwa zaidi ya shilingi Bilioni 5 katika miradi mbalimbali ya maendeleo na katika mradi wa mfereji  ambao wametembelea umegharimu kiasi cha Bilioni 3.2
“Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kwa sababu zamani kulikuwa na kero ya maji ya mvua kuingia katika makazi ya watu lakini kutokana na mradi huo kutekelezwa,suala la  mafuriko kwa kiasi kikubwa yamepungua katika mtaa huo”. Amesema Pazzi.
Aidha,  amempongeza Rais Samia kwa  kuwapatia shilingi Milioni 360 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 18 vya madarasa katika shule ya sekondari Buguruni kwani awali walipatiwa shilingi milioni 220 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa kupitia mradi wa Uviko19 na sasa hivi kwenye pochi la mama wamepatiwa milioni 120 wamejenga vyumba sita vya madarasa.

Habari Zifananazo

Back to top button