CCM, CPC kuendeleza mahusinao ya kirafiki

kusaidiana katika elimu, falsafa ya siasa, uchumi

KATIBU  Mkuu wa CCM, Ndugu Daniel Chongolo ameendelea na ziara kikazi nchini China huku akiongozana na viongozi wengine wa CCM, wakiwemo Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, Wenyeviti wa Mkoa pamoja na Wenyeviti wa Jumuiya.


Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM inalengo la kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kindugu yaliyopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomonisti cha China (CPC).


Pamoja na Mambo Mengine CCM na CPC zimejikita zaidi katika kusaidiana katika mambo ya Elimu na Mafunzo ya Falsafa ya Siasa na Uchumi.

Taarifa ya Katibu Mkuu huyo wa CCM kwa vyombo vya Habari imesema kuwa  mahusiano kati ya vyama hivyo, yameasisiwa na waanzilishi wa vyama hivyo vikongwe na kuendelea kuimarishwa na viongozi wa sasa.

Ziara hiyo imeanza April 16, 2023 na inatarajiwa kumalizika Aprili 26, 2023

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x