CCM Tanga kudili wanaosababisha migogoro

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimeweka wazi kuwa katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa hakitawabeba wenyeviti ambao wamesababisha migogoro katika maeneo yao ikiwemo ya ardhi pamoja na kutosoma taarifa za mapato na matumizi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman amesema hayo leo mkutano wa ndani wa wanachama uliofanyika katika kijiji cha Sunga Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.

Advertisement

Akieleza msimamo huo amesema kuwa chama hicho hakipo tayari kubeba wagombea ambao wakati wa uongozi wao walisababisha kero nyingi Kwa wananchi badala ya kuwa suluhu ya migogoro hiyo.

“Wewe kama ni Mwenyekiti unajijua ulikuwa unahusika na kuuza ardhi kiholela na kupelekea migogoro unahusika kwenye ubadhirifu wa mapato na fedha za miradi niseme Kwa kunywa Wazi hatutabeba wagombea wa namna hiyo, amesema Rajab.