CCM Tanga wamchangia hela ya fomu Rais Samia

TANGA: Chama Cha Mapinduzi mkoani Tanga kimechanga Sh milioni 1.7 Rais Samia Suluhu kwa ajili ya gharama ya fomu ya kugombea nafasi ya hiyo wakati wa uchaguzi utakapofika.

Akikabidhi fedha hizo kwa Katibu CCM mkoa, Seleman Sankwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kata ya Msambweni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman amesema kuwa kutokana na mazuri yaliyofanywa na Rais Samia wamevutika kumchangia gharama za ununuzi wa fomu hiyo .

“Sisi CCM Tanga tumeamua kuchangia kabisa gharama za fomu ya Rais ya kugombea nafasi hiyo pindi wakati ukifika kwani kutokana na mazuri aliyoyafanya katika nchi hii tumeona tumsaidie gharama za hizo za fomu”amesema Mwenyekiti Rajab.

Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kutekeleza ilani ya CCM kwa kiwango kikubwa hali ambayo imesaidi kupunguza kero kubwa ya huduma ambazo zilikuwa zipo kwenye sekta mbalimbali hapa nchini.

“Ndugu zangu tusiwe wachoyo wa fadhilia kwenye nchi hii sekta za elimu ,maji na nishati zimeweza kuboreshwa kwa kiasi kikubwa katika awamu hii ya sita hivyo hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea kwa Mungu Rais wetu lakini na kumchangia gharama ya fomu “alisisitiza Mwenyekiti Rajab.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Tanga ambaye ni Waziri wa afya Ummy Mwalimu alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imeweza kufanya maboresho makubwa ya huduma ya mama na mtoto katika sekta ya afya.

Ambapo alisema kuwa hivi karibuni serikali inakwenda kusambaza vifaa tiba kwa ajili ya huduma ya kujifungua kwenye hospitali zilizopo nchini lengo ikiwa ni kupunguza changamoto ya uhaba wa vifaa lakini na kuboreshewa utoaji wa huduma kwa wajawazito.

 

Habari Zifananazo

Back to top button