CCM wataja mambo yaliyochangia ushindi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetaja mambo mbalimbali yaliyochangia kushinda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Amani Zanzibar pamoja na kata zote saba zilizopiga kura kujaza nafasi za madiwani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameiambia HabariLeo kuwa sababu hizo ni umoja na mshikamano ndani ya Chama, utekelezaji wa ahadi zake, uteuzi wa wagombea bora, kampeni za kisasa zilizowafikia wapiga kura na uadilifu na uaminifu katika kuwatumikia wananchi, hususan kukidhi mahitaji na matarajio yao kwa kuwaletea maendeleo.

Shaka, amesema mambo hayo yamechochea ushindi wake Amani na kata zilizohusika na uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki.

“Kazi ambayo inafanywa kwa weledi na ustadi mkubwa na serikali zake zikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Dk. Husein Ali Mwinyi kupitia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x