CCM kutatua changamoto za wananchi
ARUSHA: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC), Itikadi, Uenezi na , CPA Amos Makalla amewasili Mkoani Arusha tayari kwa kuanza ziara yake ya siku 6 Katika Mkoa wa Arusha na Manyara.
CPA Makalla amewasili na kupokelewa mkoani humo leo Septemba 4,2024 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Sabaya pamoja na viongozi wengine wa chama wa mkoa huo.
Aidha, akiwa Mkoani Arusha atazungumza na Wananchi katikasa mikutano ya nje na mikutano ya ndani huku lengo likiwa ni kukagua Uhai wa chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi kisha kuzipatia majibu na baadaye atahamia Mkoa wa Manyara Kwa kuendelea na Ziara yake .