CCM yataka watanzania kushiriki Dira ya Taifa 2025-2050

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa rai kwa watanzania kushiriki katika kutoa maoni kwa ajili ya kuandika Dira ya Taifa ya mwaka 2025-2050.
Rai hiyo ameitoa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda leo katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
“Naomba watanzania tushiriki katika fursa hii kwakuwa dira inayoenda kuandikwa sio ya CCM, ni ya watanzania wote.
Hivyo, tushiriki kwa maendeleo ya taifa,” amesema Makonda.
Aidha amesema chama hicho kimeanzisha utaratibu na utamaduni wa kutoa ripoti ya robo ya mwaka kutoa tathmini ya utekelezaji wa ilani ya chama.
Amesema, taarifa hizo zinaegemea katika utekelezaji wa shughuli za kichama ikiwemo kufanya ziara katika mikoa na maeneo tofauti kupitia ofisi za Makamu Mwenyeki wa Chama, Komredi Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wa chama.
Amesema katika kipindi cha robo mwaka chama pia kimepanua wigo wa kidiplomasia na siasa za Kimataifa kwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na Chama cha ANC cha Afrika Kusini.
Una maoni usisite kutuandikia
Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness
#HabarileoUPDATES

