CCM yawapa pole serikali ya Algeria

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid, amewasilisha salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Algeria, Liamine Zeroual.

Rabia amewasilisha salamu hizo Aprili 1, 2026 katika makazi ya Balozi wa Algeria nchini, Gharib Zermane, ambapo pia alitia saini kitabu cha maombolezo. Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kumuenzi kiongozi huyo, anayekumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha demokrasia nchini humo.

Marehemu Zeroual alikuwa miongoni mwa wanajeshi waliopigania uhuru wa Algeria kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa mpito mwaka 1994. Mwaka 1995 alisimamia uchaguzi wa vyama vingi vya siasa na kuhudumu madarakani kwa kipindi cha miaka minne hadi Aprili 27, 1999 alipong’atuka. SOMA: Mali Algeria zalumbana kuhusu droni

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Start making cash right now… Get more time with your family by doing jobs that only require for you to have a computer and an internet access and you can have that at your home. Start bringing up to $2700-$5700+Dollar per week . I’ve started this job and I’ve never been happier and now I am sharing it with you, so you can try it too. You can check it out here…
    Here is I started_______ w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button