Chalamila: Tatizo Kagera kila mtu mwanasheria, vingereza vingiii

Chalamila: Tatizo Kagera kila mtu mwanasheria, vingereza vingiii

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, amedai kuwa Mkoa wa Kagera hauendelei kibiashara kwa sababu mbalimbali, lakini mojawapo ni wakazi wake kila mmoja kuwa mwanasheria.

Chalamila ameyasema hayo katika mkutano wa  wanachama na wananchi, ulioitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, wa kusikiliza kero za wananchi, kukagua miradi inayotekelezwa na serikali pamoja na kukagua uhai wa chama.

“Wahaya, Wanyambo watu wa Mkoa huu kila mtu mwanasheria kubishana bishana tu, vingereza vingi, sitaki vingereza.

Advertisement

“Watu wa mkoa huu wanafungua maduka saa tatu, mimi huwa sielewi hivi mnakua mmelala kweli au huwa mnafanya nini? Alihoji Chalamila.

Amewataka wakazi wa Kagera kubadilika, kwenda na mfumo wa dunia na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamba  atakuwa mstari wa mbele kufanya mageuzi makubwa ya kimtazamo, ikiwemo biashara zao kufunguliwa mapema hata kama ni Jumamosi.