TIMU ya Stend United maarufu Chama La Wana yenye maskani yake mkoani Shinyanga imezindua jezi mpya itakayotumika katika msimu huu wa Ligi ya Championiship huku ikiwa na wachezaji wake wote waliosajiliwa
Uzinduzi wa jezi hizo ulifanyika jana kwa ufadhli wa kampuni ya Jampo Food Product maarufu ‘Jamukaya.
Mwenyekiti wa mashindano wa timu hiyo, Chrispian Kwakaya amesema mashabiki walikuwa wakizubiri kwa hamu jezi hizi sasa muda umetimia kwa timu yao ya hapa nchini.
“Stend zote za hapa nchini hazina timu hivyo timu yao ni stend United ambayo ni chama Lawana hivyo tumezindua leo kufurahisha mashabiki ili wote wazipate kwa bei “amesema
Kocha wa timu hiyo Meja Mstaafu Abdul Mingange amesema wachezaji leo wamepumzika tayari kwa mchezo wa kesho wanawafurahisha mashabiki watashinda.
“Mchezo uliopita haukuwa mzuri ila wachezaji wako vizuri kiakili na kimwili tunaomba kushinda ila Ligi ya Championiship mimi ninauzoefu nayo changamoto kwenye timu zinazoshiriki l ligi hii ninazifahamu”amesema Mingange.
Kaptein wa timu hiyo Gables Chitemba ameomba mashabiki wajitokeze kwa dhati kwani watakapozinunua jezi watakuwa wametumia uzalendo wa ndani ya mkoa nan chi kwa ujumla ambapo wameahidi watafanya vizuri msimu huu nakupanda daraja.
Kupitia uzinduzi huo wamewatambulisha bechi la ufundi,Washambuliaji, wakabaji na walinda mlango watatu (Golikipa).
Timu ya Stand United inatarajia kuingia uwanjani kesho kuendelea na ligi ya Championiship kuvaana na timu ya Bigman ambayo zamani ilijulikana kama Mwadui Fc.