Chama Tawala chaongeza viti vya wabunge

CHAD : CHAMA tawala cha Patriotic Salvation Movement (PSM) kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge wa mwezi Desemba nchini Chad, ambapo kimejizolea viti 124 kati ya 188.
Uchaguzi huu, ambao ulisusiwa na vyama vikuu vya upinzani, umeonekana kuwa na athari kubwa katika kuimarisha nguvu za kisiasa za Rais Mahamat Idriss Deby.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Ahmed Bartchiret amesema idadi ya wapiga kura ilifikia asilimia 51.5, ishara kwamba ingawa upinzani ulikusudia kuonyesha kutoridhishwa na uchaguzi huo, umoja wa chama tawala umedhihirika kwa kiwango kikubwa.
Uchaguzi wa bunge pamoja na uchaguzi wa serikali za mitaa na mikoa, ni sehemu ya mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia baada ya Rais Mahamat Idriss Deby kuchukua madaraka kama rais wa kijeshi mwaka 2021.
Aliingia madarakani baada ya kifo cha baba yake, Rais Idriss Deby Itno, ambaye aliongoza Chad kwa miongo mitatu. SOMA: Jen. Deby aahidi kuwamaliza Boko haram
Kwa ushindi huu, chama tawala kinaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika mchakato wa kisiasa nchini Chad, na wengi wanatarajia kuwa hatua hii itaimarisha zaidi nguvu za Rais Mahamat Deby katika kipindi cha mpito.



