CHAD : RAIS wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby amesema Jeshi la Chad limefanya mashambulizi ya anga na kuwauwa na kuwajeruhi wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram.
Akizungumza na waandishi wa habari, Deby amesema mashambulizi hayo yamefanyika baada ya wanamgambo hao kulishambulia jeshi la Chad mwezi uliopita katika eneo la magharibi karibu na mpaka wa Nigeria na kuwauwa takriban watu 40 na kuwajeruhi watu wengine kadhaa.
Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa mpito Abderahim Bireme Hamid alitamka kuwa, operesheni ya jeshi la Chad dhidi ya wanamgambo hao inalenga si tu kuhakikisha amani kwa raia bali pia kuwakamata Boko Haram na washirika wake wanaoendelea kusababisha madhara kwa raia wa nchi hiyo.
SOMA: Rais mpya Chad aapishwa