Chelsea yajiweka sawa kumsajili Kobbie Mainoo
CHELSEA iko tayari kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United, Kobbie Mainoo, katika dirisha la usajili mwezi huu iwapo mchezaji huyo ataonesha nia kuhamia klabu hiyo.
Mapema wiki hii, tetesi zilidai Chelsea ilikuwa ikiongoza mbio kumsajili Mainoo huku kukiwa hakuna maendeleo katika mazungumzo kuhusu mkataba mpya Old Trafford.
Wakati mpango wa Chelsea kwa Mainoo unaonekana kulenga dili la bei nafuu, uhamisho unaweza kufanyika mapema mwezi huu iwapo Mainoo ataonyesha nia.
Mainoo ana mkataba na Manchester United hadi 2027, huku kipengele cha kuongeza mkataba kwa miezi 12 kikimbakisha mchezaji huyo hadi 2028.



