China wekezeni Tanzania – Prof Mkumbo
CHINA : WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Alexander Mkumbo akihutubia katika kongamano la Thought Leadership on China- Africa Trade and Investment Forum lililoandaliwa Benk ya Viwanda na Biashara ya China, jijini Beijing.
Kongamano hilo ni miongoni mwa shughuli mbalimbali zinazofanyika pembezoni mwa mkutano wa FOCAC, na limelenga kuhamasisha uwekezaji katika sekta za miundombinu, madini, nishati na kilimo kwenye nchi za Afrika.
Aidha, Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Nchi walioalikwa, Mawaziri na Maafisa Waandamizi pamoja na Wawekezaji na Taasisi za Kifedha za kimataifa.
SOMA : Tanzania, China kushirikiana matibabu ya moyo
Prof. Mkumbo amepata nafasi ya kueleza kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini, huku ujumbe wa Tanzania ukipata fursa ya kukutana na wawekezaji wakubwa katika sekta za miundombinu, madini, nishati na kilimo,