Chongolo uso kwa uso na bilionea Laizer.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo amekutana na bilionea Laizer katika mkutano wa shina namba 26 Tawi la Naisinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kumpongeza kwa kuchangia maendelea katika wilaya hiyo.

Bilionea Laizer ni moja ya wanachama wa CCM katika shina na tawi hilo, ambalo Chongolo leo amefanya mkutano katika Tawi hilo kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa eneo hilo kwa kutoa maelezo mbalimbali kwa serikali ikiwemo uboreshaji wa barabara, maji na mifugo na mawasiliano.

Laizer katika eneo hilo amejenga shule ya msingi ya inayofundisha kwa kutumia Lugha ya Kiingereza kwa lengo la kuinua elimu kwa wananchi wa eneo hilo.

Advertisement

Katibu Mkuu yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani, kuimarisha uhai wa chama pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Sofia Mjema na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Issa Gavu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *