Choplife Gaming Limited usukani wa maendeleo michezo kubahatisha

Choplife Gaming Limited, kampuni yenye haki za usimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania ambayo pia inaendesha biashara zake Mashariki na Magharibi ya Afrika, inaendelea kufanya vyema katika soko la michezo hiyo nchini.
Ikiwa na machaguo mbalimbali ya michezo ya kubahatisha ikiwamo; ubashiri kwenye michezo, casino na michezo ya video, kampuni hiyo imeendelea kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vya ubora, ufanisi na sheria na kanuni zinazoongoza tasnia hiyo.
Hivi karibuni, Choplife Gaming Limited ilipokea tuzo ya “Mlipa kodi Mkubwa wa Ujumla” kwa ukanda wa Mashariki nchini kutoka kwa waandaaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Heshima hii iliyopatikana inadhihirisha jitihada za dhati zisizomithilika za ulipaji kodi na uchangiaji katika ukuzaji uchumi wa nchi na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Akizungumzia mafanikio hayo, Mwenyekiti wa Kampuni ya Choplife Gaming Limited, Oluwatosin Ajibade, alieleza kufurahishwa na hatua hiyo, akisema: “Tumefarijika kupokea tuzo hii. Inatupa hamasa ya kuendelea kuwekeza zaidi barani Afrika.
Ikiwa ni kampuni inayomilikiwa kihalali na Waafrika, tunapambana kuhakikisha Afrika inakuwa sehemu bora na njia mojawapo ya kufanikisha hili ni kupitia kulipa kodi kwa uaminifu katika mipaka yote ya kisheria tunayofanyia kazi, ikiwamo Tanzania.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa TRA kwa mchango wao, pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira bora kwa wawekezaji.
“Mazingira hayo yametuhamasisha kutanua uwekezaji wetu kila kona ya Tanzania ikiwamo michezo ya ubashiri ambayo ndiyo iliyoleta tuzo hiyo. Kwa pamoja, tunaweza kuifanya Afrika kuwa bora zaidi.”

Mkurugenzi wa Choplife Gaming Limited, Loyce Oluoch (kushoto) na Meneja Fedha wa Choplife Gaming Limited, Albano Mhando (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na tuzo yao ya Mlipa Kodi Mkubwa wa Ujumla waliyoshinda katika Tuzo za Mlipa Kodi 2023/24 zinazoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia, anasema: “Ushindi huu ni ishara ya ufanyaji kazi kwa ubora na uadilifu. Kwa wateja wetu, inaongeza imani kwetu kuwa kampuni tegemeo kwao. Kwa wadau, inadhihirisha nafasi yetu kama mshirika wa kutumainiwa katika maendeleo ya Tanzania. Na kwa uongozi na wafanyakazi wetu, ushindi huu ni motisha tosha ya kuendelea kuongoza kwa mfano na hamu ya kuyaendea mafanikio zaidi.”
Anasema kuwa kuipata tuzo hiyo katikati ya mikakati yao ya kuendelea kudumisha viwango ya hali ya juu vya utendajikazi, lilikuwa jambo lisilotegemewa.
“Inadhihirisha nguvu ya pamoja ya wafanyakazi wetu na utayari wetu wa kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania,” anasema Mwenyekiti huyo.
Uwekezaji katika kufanya kazi kwa bidii na kujiweka karibu na jamii zinazowazunguka, kumechangia kuimarisha nafasi yake ya uongozi wa soko la michezo ya kubahatisha nchini.
Kupitia kampeni zake za uhamasishaji ushiriki/uchezaji kwa kiasi wa michezo ya ubashiri na shughuli za urudishaji kwa jamii, kampuni hiyo bado iko mstari wa mbele wa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya ukanda mzima.
Akiulizwa kuhusu uzoefu wa tuzo za TRA za mwaka 2023/24, alipongeza uandaaji wa tuzo hizo, akiamini kuwa tuzo hizo ni jukwaa la kutambua mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi.
Pongezi hazikuishia hapo, pia alisema: “Tukio zima liliandaliwa vizuri, huku lengo likiwa ni kusherehekea ulipaji kodi kwa hiari, ubunifu na uchapakazi kwenye maeneo mbalimbali. Ilikuwa heshima ya aina yake kushuhudia na kushiriki katika tuzo hizo zenye msisimko ukizungukwa kwa karibu na kampuni kubwa zilizopo katika soko hilo.”
Jambo lingine linalozifanya tuzo hizo kuwa za mfano ni uwezo wake wa kushawishi kampuni kujiendesha kwa kuzingatia maadili na malengo ya maendeleo ya Taifa.
Rais Samia Suluhu Hassan akikabidhi kwa Mkurugenzi wa Choplife Gaming Limited, Loyce Oluoch wakati wa Tuzo za Mlipa Kodi 2023/24 zinazoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kampuni hiyo iliibuka kuwa Mlipa Kodi Mkubwa wa Ujumla.
Mbali na hilo, uwazi wa mchakato wa uchaguzi wa washiriki na uzingatiaji makundi ya aina zote unazifanya tuzo hizo kuaminika na kuwa jumuishi zaidi.
“Hapo mbeleni, waandaaji wanaweza kufikiria kutengeneza majukwaa shirikishi zaidi wakati wa ufanyikaji wa tuzo husika ambapo washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na ujuzi.
Kwa mara nyingine tena, tumefurahi kupata tuzo hii, na tuna imani kuwa bado tutaendelea kuleta mabadiliko chanya katika jamii,” amebainisha.



