MICHEZO mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara inafanyika viwanja tofauti leo.
Bingwa mtetezi Yanga ipo mkoani Arusha ikiwa mgeni wa Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Yanga ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 6 wakati Coastal Union ni ya 10 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 8.
SOMA: Yanga kama hawapo vile!
Katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wenyeji Dodoma Jiji inawakaribisha JKT Tanzania.
JKT Tanzania ni ya 8 ikiwa na pointi 10 baada ya michezo 8 wakati Dodoma Jiji inashika nafasi ya 9 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 8 pia.
KMC ya Dar es Salaam imesafiri hadi Mbeya kuwavaa wenyeji maafande wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine.
KMC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 8 wakati Tanzania Prisons ni ya 12 ikiwa na pointi 7 baada ya idadi kama hiyo ya michezo.
Comments are closed.