TIMU ya Coastal Union leo imeibuka mshindi kwa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mabao ya Coastal katika mchezo huo wa pili kupata ushindi tangu Ligi Kuu kuanza yamefungwa na Maulid Maabad dakika ya 2 wakati la pili limefungwa na Hernest Malonga dakika 88.