KLABU ya Coastal Union ya Tanga imetangaza kutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani.
Coastal ilikuwa ikitumia uwanja wa KMC, Dar es Slaam ajili ya mechi zake za nyumbani kutokana na uwanja wa muda mrefu wa Mkwakwani jijini Tanga kuwa katika maboresho.

“Uongozi wa Coastal Union unapenda kuwajulisha rasmi mashabiki na wadau kwamba timu yetu itatumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kama kiwanja chetu cha nyumbani kwa michezo yetu inayofuata,” imesema taarifa ya timu hiyo.
Coastal inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 7.