Watu 27 wapoteza maisha Congo

CONGO : SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza iko katika hali ya tahadhari kutokana na ugonjwa usiojulikana ambao umesababisha vifo vya watu kadhaa nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa nchini humo,Waziri wa afya Samuel Roger amesema mamlaka bado zinaendelea kufuatilia mlipuko wa ugonjwa huo.
“Mpaka sasa kuna watu 27 ipo katika vituo vya afya ambao wamethibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo”. Alisema. SOMA: Ugonjwa usiojulikana wazuka Congo
Ugonjwa huo unasababishwa na dalili za mafua makali ambazo ni homa, kikohozi na maumivu ya kichwa.
Kwa mara ya kwanza ugonjwa huo uligundulika mwishoni mwa mwezi Oktoba, na hadi sasa umeripotiwa zaidi katika eneo la Panzi, takriban kilomita 700 kusini mashariki mwa mji mkuu Kinshasa.
Kamba ameongeza kuwa watu wengine 44 wameripotiwa kufariki lakini hawajathibitisha vifo hivyo vimesababishwa na ugonjwa huo.



