CONGO: NAIBU gavana wa mkoa wa Kwango, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Remy Saki na waziri wa afya wa nchi hiyo Apollinaire Yumba wametangaza hali ya tahadhari kwa kuzuka ugonjwa mpya usiojulikana Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.
Taarifa zinasema watu wengi walioambukizwa walikuwa na dalili za kuugua mafua pamoja na kupata joto kali mwilini na kuumwa kichwa. SOMA: DRC kupatiwa chanjo ya Mpox
Kwa mujibu wa maafisa hao wa ngazi za juu Congo, timu ya madaktari imeshachaguliwa na kupelekwa katika eneo hilo ili waweze kuchukua sampuli kuchunguza zaidi ugonjwa huo.
Wakatihuohuo, kiongozi mmoja anayetoka shirika la kiraia, Cephorien Manzanza amesema hivi sasa kumekuwepo na wasiwasi mkubwa katika eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu walioambukizwa ambao wengi ni wanawake na watoto.