CONGO: Mapigano yameanza tena kusini mwa Kivu

CONGO : MAPIGANO yamezuka tena kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kusini mwa Kivu, licha ya tangazo la waasi la kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu.

Ripoti kutoka eneo la Nyabibwe, mkoani Kalehe, zinasema kuwa mapigano yaliendelea mapema leo baada ya waasi wa M23 kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na serikali. Jumatatu, waasi walitangaza kusitisha mapigano na kusema kuwa hawakuwa na nia ya kuchukua maeneo yoyote baada ya kuteka mji wa Goma.

Hata hivyo, mamlaka ya DRC inasema shambulio hilo linakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotolewa na waasi siku mbili zilizopita. Baada ya kuushikilia mji wa Goma, waasi wa M23 walikusudia kuteka mji wa Bukavu, mji mkubwa zaidi katika mkoa wa Kivu Kusini, lakini walikumbana na upinzani mkali kutoka kwa vikosi vya serikali ya Congo na Burundi, ambao walirejesha vijiji kadhaa vilivyokuwa vimetekwa na waasi.

Serikali ya DRC imeanzisha juhudi za kusajili raia kujiunga na vikosi vya jeshi ili kuimarisha ulinzi wa Bukavu na maeneo mengine yaliyo hatarini katika jimbo la Kivu Kusini.

SOMA: Serikali ya DRC yathibitisha uwepo wa Rwanda Goma

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button