Congo yaomba Rwanda kuwekewa vikwazo

CONGO: JAMHURI ya Kidemokrasi ya Congo imetoa wito Rwanda iwekewe vikwazo na kupunguziwa misaada na pia isimamishwe ushiriki wake katika misheni za kulinda amani UN kwa jukumu ambalo inadaiwa kutekeleza katika mzozo wa Congo Mashariki.
Waziri wa mambo ya nje wa Congo Therese Kayikwamba aliiambia BBC, Rwanda inakalia eneo la nchi yake kinyume cha sheria.
Therese amesema Rwanda inaunga mkono, kufadhili na kuandaa ujasusi ambao unatafuta kupindua serikali iliyochaguliwa kisheria.
Wakijibu suala hilo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema nchi yake inatetea mipaka yake wala haina nia ya mabadiliko ya serikali.
Viongozi wa waasi ambao walichukua udhibiti wa baadhi ya sehemu za Jiji la Goma wiki hii walisema Alhamisi kwamba wanakusudia kufika Kinshasa.
SOMA: Rwanda,Marekani wakubaliana kumaliza mgogoro Congo


